background
udsm logo
udsm_logo
heet_logo

UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

Higher Education for Economic Transformation (HEET) project

logo
Home

FURSA ZA UWEKEZAJI NA UTOAJI WA HUDUMA KATIKA KAMPASI MPYA YA UDSM LINDI

Tue Sep 29 2026

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinapenda kuufahamisha umma, taasisi za umma na binafsi, makampuni, wafanyabiashara na watoa huduma kuhusu fursa za uwekezaji na uendeshaji wa biashara zinazopatikana katika Kampasi mpya ya UDSM Lindi, iliyopo eneo la Ngongo, Manispaa ya Lindi, Mkoa wa Lindi.

Kampasi inatarajiwa kuanza shughuli za kitaaluma katika mwaka wa masomo 2026/2027 ikiwa na takribani wanafunzi 120 katika hatua ya awali, pamoja na watumishi, wageni na watumiaji wengine wa Kampasi. Kadiri shughuli za Kampasi zitakavyopanuka, idadi ya watumiaji na mahitaji ya huduma mbalimbali yanatarajiwa kuongezeka.

Katika maandalizi ya kuanza kwa shughuli za Kampasi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa jamii ya Chuo, UDSM inawaalika watu binafsi, makampuni na wafanyabiashara wenye sifa, uwezo na nia ya kuendesha biashara katika Kampasi kuwasilisha maombi yao. Kuna makundi mawili ya uwekezaji: kundi la kwanza ni fursa ambazo zinaombwa kwa kujaza fomu maalum  na kundi la pili ni fursa zinazoombwa kupitia Mfumo wa Taifa wa Ununuzi kwa Njia ya Kielektroniki (NeST)

Makundi maalum (vijana, wanawake na wenye ulemavu) wanahamasishwa kushiriki katika fursa hizi.

bg
udsm_logoheet_logo
Revolutionizing High education for Economic transformation.
Contact Us
Call Us:
+255 765 939 958
Email:
heet@udsm.ac.tz
© 2026 University of Dar es Salaam - Higher Education For Economic Transformation Project
Term of use / Privacy Policy